• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirikiano
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Legal
      • Mkaguzi Wa Ndani
      • ICT and Public Relations
      • Procurement and Supplies
      • Election
      • Bee Keeping
  • Fursa za uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za upimaji
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kijamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Hifadhi ya Picha
    • Maktaba ya video

Wananchi washiriki sherehe za maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani

Posted on: March 9th, 2017


Wananchi wa wilaya ya kwimba mkoani Mwanza wameshiriki sherehe za Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tarehe 08/03/2017 ikiwa na kauli  mbiu “ Tanzania  ya viwanda  wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi”

Madhimisho yameanzia viwanja vya Halmashauri kupitia viunga mbalimbali vya mji wa Ngudu hadi  viwanja vya mpira wa miguu KWIDECO na kupokelewa na mgeni rasmi ndugu Andrea Ng’wani kwa niaba ya mkuu wa wilaya.

"Mnaombwa kukemea na kuacha vitendo vya kuwazuia watoto wa kike wasipate elimu ili kuwaozesha. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya tano imeweka mpango wa makusudi kabisa  katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu ya msingi na kuendelea hasa mtoto wa kike, na ina kaulimbiu inayosema Elimu bure, hivyo kila mtoto apelekwe shule kwa wakati na asikatizwe masomo yake kwa sababu zisizokuwa na msingi, ikiwemo kuwaozesha katika umri mdogo na kuwafanya walezi wa familia. Serikali ipo makini katika kuzuia mdondoko wa watoto wa kike shuleni na kupambana na mimba za utotoni”

Hayo yamesemwa na Ndg Andrea Ng`wani katibu Tawala wa Wilaya kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya kwimba wakati akiwahutubia wananchi  na amesisitiza  kwa kusema

Mzazi yeyote au Jamii itakayohusika kwa namna yoyote ile kumkatiza mtoto wa kike masomo Sheria itachukua mkondo wake.

 Wakati wa akisoma Risala kwa mgeni Rasmi Bibi Getrude Nokingile  amesema Wanawake wengi hasa wazee na vikongwe waishio vijiji wanaishi pekee yao na wanaishi katika mazingira hatarishi,ambayo yanawafanya waonekane tofauti na watu wengine na baadhi ya watu kuhisi kwamba kutokana na hali duni ya maisha wanayoishi ni wachawi, ndio wanaosababisha vifo vya watu katika maeneo wanayoishi.Tunaomba serikali kuanzia ngazi ya kitongoji hadi ngazi ya Wilaya kushirikiana na wananchi katika kuwatambua na kuwalinda ili waishi kwa usalama na  amani.

Mwanamke ni mlezi wa familia, ni msingi wa maendeleo na ni kiongozi shupavu wa famililia hayo yamesemwa na Ndugu Innocent Sililo mkazi wa mtaa wa chamhela wilayani kwimba wakati wa  sherehe hizo.

Aidha Bibi Sobi Masalu mamaye ni mkuu wa Kitengo cha Sayansi kimu  Idara ya Elimu Msingi amesisitiza kuwa ili mwanamke aweze kukidhi kauli mbiu ya mwaka huu anahitaji Elimu ya ujasiliamali, Mtaji, mfumo dume kuondolewa, stadi za ujuzi mbalimbali na hasa za maendeleo zifundishwe kwa msisitizo  kuanzia madarasa ya chini na somo la S/Kimu lirudishwe shule za msingi ili mtoto anapomaliza elimu ya msingi awe na maarifa ya kumwezesha kupambana na mazingira yanayomzunguka.

Maadhimisho hayo yamehitimishwa kwa kuwapa vyeti walimu wa kike kumi  katika shule za Msingi na Sekondari wilayani humo ambao  wamefaulisha vizuri mitihani ya Taifa 2016/2017.

Matangazo

  • Tangazo la kazi Watendaji wa Vijiji (nafasi 55) April 06, 2018
  • Tangazo la Kazi ya Wauguzi February 06, 2018
  • Tanzia January 17, 2018
  • Tangazo la Kupata Mafundi Katika Kituo cha Afya Malya January 16, 2018
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • Watoa huduma watakiwa kuzingatia mafunzo ya mifumo ya kielektronikia

    March 19, 2018
  • DC-Kwimba Auomba Uongozi wa Wilaya Kutambua Wajibu Wake Katika Kutekeleza Mradi wa Mama na Mtoto

    January 24, 2018
  • Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Umefanya Ziara ya Kutembelea Kituo cha Afya Kahangala na Karume

    January 08, 2018
  • Wadau Mbalimbali wa TLB Kwimba Wafanya Kikao cha Kimkakati

    January 05, 2018
  • Onyesha zote

Video

Marufuku ya Michango Shuleni
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Raisi Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Raisi utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Raisi Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.