• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

DC KWIMBA AZINDUA UTOAJI KINGA TIBA YA POLIO

Posted on: May 18th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Mussa Samizi leo tarehe 18,Mei 2022 amefanya uzinduzi wa Chanjo ya polio kwa watoto wenye miaka sifuri hadi mitano, uzinduzi huo umefanyika katika maeneo tofauti ya Tarafa ya Mwamashimba.


Katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya amepata fulsa ya kuwapatia watoto matone ya chanjo ya polio katika Zahanati ya Kikubiji na Kituo cha Afya Mwamashimba. Pia mkuu huyo ametembelea kaya mbalimbali za Wananchi wa Mwashimba ili kukagua utekelezaji wa utoaji wa Chanjo za polio.


Kampeni hii ya utoaji wa Kinga tiba ya polio imeanza leo hadi tarehe 21 Mei, 2022. Zoezi la utoaji wa kinga linafanyika Nyumba kwa Nyumba ambapo wahudumu wa Afya wanapita kutoa kinga hizo, vilevile kinga hizo zinatolewa katika Zahanati na Vituo vya Afya


Aidha katika kuhakikisha Elimu inawafikia wazazi kwa wingi Mkuu wa Wilaya ya Kwimba amefika Shule ya Msingi Kikubiji na kuongea na Wanafunzi wa Shule hiyo ambapo amewataka kwenda kuwa mabalozi ili ujumbe huo wa kinga kwa watoto uwafikie wazazi wote ili wawe tayari kuwatoa watoto wao kupata kinga.


Akiongea na Wanafunzi hao Mheshimiwa Samizi amesema madhara ya watoto kutopata kinga ya polio ni makubwa kwani ugonjwa wa polio hauna tiba na ukishampata mtoto anapooza na kupelekea ulemavu.


"waambieni wazazi wenu wawapeleke wadogo zenu kupata chanjo ya polio ili wawaepushe na madhara yanayoweza kujitokeza hasa ugonjwa wa kupooza, tena wasisitizeni kuwa ugonjwa wa polio hauna dawa kwahiyo mtoto akiupata ni hatari kubwa kwake na kwa watoto wanaomzunguka" amesema Samizi

Matangazo

  • MKUTANO WA KUELEZEA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA WA MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU March 18, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA AJIRA YA VEO May 19, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA AJIRA YA VEO May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI May 24, 2022
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • DC SAMIZI AAGIZA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA 2023 KURIPOTI SHULENI KWA WAKATI

    December 27, 2022
  • DC SAMIZI AAGIZA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA 2023 KURIPOTI KWA WAKATI SHULENI

    December 27, 2022
  • MADIWANI WANG'AKA WATAKA WADAIWA SUGU FEDHA ZA MIKOPO 10% KUKAMATWA

    December 15, 2022
  • WATOA HUDUMA ZA MAJI WATAKIWA KUSIMAMIA VYANZO VYA MAJI

    December 14, 2022
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.