Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya kanda ya Afrika Prof. Mohamed Yakub Janabi amezindua jengo la watoto wachanga leo 28, Februari 2026 Wilayani Kwimba
" uzinduzi wa jengo hili kwa shirika la Afya Duniani ni zaidi ya jengo, ni ushahidi kwamba wananchi wanapata huduma katika mazingira sahihi"
Janabi ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuboresha huduma za Mama na Mtoto, shirika linataka vifo vya mama na mtoto vipungue zaidi kufikia mwaka 2030 kuwe na vifo sabini kati ya vizazi laki moja" Janabi
Amesisitiza kuwa kwa bara la Afrika bado changamoto ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano ni kubwa ambapo shirika la Afya linaendelea kujipanga kupunguza vifo hivyo.
Aidha amewapongeza wafadhili Keepa a child alive (KCU) na Doris Foundation kwa kuona umuhimu wa kujenga jengo hilo ili kupunguza vifo vya watoto wachanga.
"mmejenga urithi wa matumaini, kituo hiki kinamaanisha uzima wa mtoto ni jukumu letu sote"amesema Janabi
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mkurugenzi wa Shirika la Doris Mollel Foundation Bi. Doris amesema mradi huo aliuanzisha baada ya kufika Kwimba kuleta vifaa tiba na kugundua watoto njiti hawana Wodi maalumu ya kutoshereza mahitaji hivyo akaamua kutafuta wadau waliowezesha ujenzi huo.
Doris ametumia nafasi hiyo Kumshukuru mdau kutoka KCU kwa kukubali kufadhili ujenzi wa jengo na vifaa tiba jengo ambalo ni la kisasa na linakwenda kutatua changamoto kwa watoto njiti.
Naye Antonio Luis Mkurugenzi wa Shirika la KCA amesema shirika hilo linafanyakazi ya kuhakikisha watoto wanakuwa salama na walifurahia kupata wazo la kujenga jengo hilo kutoka kwa Doris Foundation " miaka michecha nilikuja Tanzania na nikashuhudia baadhi ya wazazi na watoto wachanga nikapata wazo la kujenga jengo hili, tuko hapa ni kwasababu tunataka kuona watoto njiti wakipata matibabu katika mazingira mazuri" amesema Antonio
Pia Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Cosmas Bulala amempongeza Doris kwa ujenzi wa jengo hilo na amemuahidi kulinda miundombinu ya jengo hilo " leo ni uzinduzi wa matumaini mapya kwa watoto wanaozaliwa Kwimba" amesema
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.