• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

WANANCHI WA KATA YA KIKUBIJI WASHIRIKI UCHIMBAJI WA MSINGI UJENZI WA KITUO CHA AFYA

Posted on: August 16th, 2022

Kata ya Kikubiji ni miongoni mwa kata tatu za  Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba zilizopata fedha kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya. Jumla ya shilingi milioni 500 zimeshapokelewa kwaajili ya ujenzi wa Kituo hicho, ambapo awamu ya kwanza ilipokelewa milioni 250 ambazo zimetumika kujenga majengo matatu yaani jengo la wagonjwa wa nje. ( OPD), Maabara na kichomea taka.

Fedha zilizopokelewa awamu ya pili ni milion 250 ambapo majengo matatu  yanatarajiwa kujengwa  jengo  la wazazi,jengo la upasuaji na jengo la kufulia.


Kutokana na mapokezi ya fedha hizo za awamu ya pili wananchi wakishirikiana na watumishi wa Halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi.Happiness Msanga wamechimba msingi wa majengo hayo matatu huku wakiishukuru Serikali kwa kuendelea kuleta fedha za miradi katika kata hiyo.

“ tunaishukuru Serikali kwa kutuletea fedha za kujenga hiki kituo cha Afya, kata hii tulikuwa hatuna kituo cha Afya kitu kilichokuwa kinapelekea wagonjwa wetu kupelekwa kata ya Bupamwa Kituo cha Mwamashimba kwahiyo kujenga  kituo hapa kwetu tumefurahi sana na tunaishukuru Serikali” amesema Mali ya Tabu Kasanga

Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa vituo vya Afya vinne, ambapo vitatu vimepokea fedhaza ujenzi huo katika awamu ya sita ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani na kituo kimoja kimepokea fedha za ukamilishaji.

Aidha Halmashauri inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo huduma za wagonjwa wa nje yaani OPD zinaendelea kutolewa huku ukamilishaji wa majengo mengine yakiwemo majengo ya wodi, jengo la huduma za  dharura na jengo la upasuaji yakiwa hatua za mwisho za ukamilishaji.

Sekta hiyo ya Afya imeendelea kuboreshwa, jumla ya zahanati nne zimepokea fedha za ukamilishaji milioni 200, huku Halmashauri kwa kutumia mapato ya ndani ikiendelea kukamilisha zahanati mbili kwa milioni 100



Matangazo

  • MKUTANO WA KUELEZEA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA WA MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU March 18, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA AJIRA YA VEO May 19, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA AJIRA YA VEO May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI May 24, 2022
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • DC SAMIZI AAGIZA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA 2023 KURIPOTI SHULENI KWA WAKATI

    December 27, 2022
  • DC SAMIZI AAGIZA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA 2023 KURIPOTI KWA WAKATI SHULENI

    December 27, 2022
  • MADIWANI WANG'AKA WATAKA WADAIWA SUGU FEDHA ZA MIKOPO 10% KUKAMATWA

    December 15, 2022
  • WATOA HUDUMA ZA MAJI WATAKIWA KUSIMAMIA VYANZO VYA MAJI

    December 14, 2022
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.