• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

WATENDAJI WATAKIWA KUKUSANYA MAPATO KWA UAMINIFU

Posted on: November 11th, 2022


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewaelekeza watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato kwa uaminifu.

Ameyaelekeza hayo leo tarehe 11,Novemba 2022 kwenye kikao cha Robo ya kwanza ya mwaka cha Watendaji wa kata na vijiji kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu

“ukusanyaji wa mapato siyo jambo la hiari, ni takwa la kisheria kwahiyo iwe jua iwe mvua lazima tukusanye mapato” amesema Msanga

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa ukusanyaji wa mapato ni jukumu la watumishi wote hasa watendaji wa vijiji na kata japo kuna baadhi ya watendaji ambao hawatimizi wajibu huo.

Aidha amekemea  baadhi ya watendaji ambao siyo waaminifu katika kukatia ushuru “ baadhi yenu siyo waaminifu mnaungana na wafanyabiashara kudanganya takwimu za mazao mnayokatia ushuru acheni tabia hiyo mara moja na tunaendelea kutafiti tutakayemkamata tutamchukulia hatua za kisheria”

Katika kikao hicho watendaji wameelekezwa kuhamasisha lishe bora hasa kwa watoto na wanawake wajawazito “hakikisheni lishe bora inakuwa agenda ya kudumu  kwenye mikutano yenu, tena naelekeza shule zote ziwe na shamba la viazi lishe au mahindi lishe na mbogamboga ili wanafunzi wapate chakula shuleni”amesema  Johari Samizi Mkuu wa Wilaya ya Kwimba


Akiwasilisha taarifa ya lishe Ya robo Mratibu wa Lishe Emma Kalolo ameeleza athari za ukosefu wa lishe bora kuwa ni  watoto kuzaliwa wakiwa na mdomo sungura, kichwa kikubwa, tumbo kubwa na magonjwa mengine na udumavu.

Watendaji walioshiriki kikao hicho wameahidi kwenda kutekeleza maagizo hayo ikiwa ni pamoja na kuibua mikakati mingine ya kuongeza ukusanyaji wa mapato

“ maelekezo tumeyapokea, tutaongeza juhudi katika kukusanya mapato ikiwa ni pamoja na kuibua vyanzo vipya na kusimamia vyanzo vilivyopo” amesema Salum M.Salum Mtendaji wa Kata ya Hungumalwa








Matangazo

  • MKUTANO WA KUELEZEA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA WA MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU March 18, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA AJIRA YA VEO May 19, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA AJIRA YA VEO May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI May 24, 2022
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • DC SAMIZI AAGIZA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA 2023 KURIPOTI SHULENI KWA WAKATI

    December 27, 2022
  • DC SAMIZI AAGIZA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA 2023 KURIPOTI KWA WAKATI SHULENI

    December 27, 2022
  • MADIWANI WANG'AKA WATAKA WADAIWA SUGU FEDHA ZA MIKOPO 10% KUKAMATWA

    December 15, 2022
  • WATOA HUDUMA ZA MAJI WATAKIWA KUSIMAMIA VYANZO VYA MAJI

    December 14, 2022
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.